Shirika la Wakarmeli (O.Carm) lipo Tanzania tangu mwaka 2009. Juhudi za kuanzisha misheni ya Wakarmeli nchini Tanzania zilianza mwaka 1988 wakati kundi la vijana kutoka Tanzania lilipo kwenda nchini Italia kwa ajili ya malezi ya kitawa na masomo ya falsafa na teolojia. Walilewa na Carmine Maggiore "La Vergine Bruna", Napoli, Italia. Baada ya kipindi cha malezi na masomo, walirejea nchini mwao tarehe 01 .10.2009 kwa ajili ya kuzindua rasmi misheni. Konventi yao ya kwanza iko Bunju "A" katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam.
Konventi ya kwanza.
Juhudi za kuanzisha shirika la Wakarmeli nchini Tanzania zilianza toka mwaka 1988. Vijana wa kitanzania walikwenda kusoma na kufanya malezi Italia. Baada ya kipindi cha masomo walianzisha rasmi misheni tarehe 1.10.2009 huko Bunju "A". Konventi ilibarikiwa tarehe 8.10.2009 na Mhashamu Askofu Methodius Kilaini, aliyekuwa askofu msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Mapadre wakarmeli wanafanya kazi katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam katika Parokia ya Bikira Maria wa Mlima Karmeli iliyotangazwa parokia tarehe 24.8.2012 wakati wa upadrisho wa Padre Dominic John Somola.
Wakarmeli watanzania chini ya Komisarieti la Bruna
Mapadre wakarmeli watanzania (O.Carm) walifungua nyumba ya kwanza ya kitawa hapa Tanzania katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam mwaka 2009. Nyumba hii (konventi) ni matunda ya kazi ya kimisionari inayosimamiwa na Komisarieti Kuu ya “Santa Maria «La Bruna»” yenye makao yake Napoli, Italia. Jambo la kufurahisha na la kutia moyo ni kuona kuwa, watawa walioifungua nyumba hii ya kwanza ya kimisionari ni wakarmeli watanzania. Walilelewa na kusomea kule Napoli Italia. Baada ya malezi, walirejea hapa Tanzania kwa ajili ya kuanzisha Shirika la wakarmeli.Maandalizi ya kufungua misheni
Mapadre waitaliano wa Komisarieti ya “Santa Maria La Bruna” walipata wazo la kuanzisha misheni hapa Tanzania tangu mwaka 1988, baada ya kupokea barua kutoka kwa Masista Wakarmeli ambao ndiyo kwanza walikuwa wamefika hapa Tanzania mwaka 1984 kwa ajili ya kuanzisha misheni yao. Katika barua hiyo, Masista waliwashauri mapadre wa Napoli waanzishe misheni Tanzania.
Mapadre walilipokea wazo hilo kwa utayari, lakini wakati huo huo walikuwa wakikabiliwa na uhaba wa mapadre. Ijapokuwa wazo lilikuwa zuri, walishindwa kulitekeleza upesi kutokana na uhaba wa mapadre waliokuwa nao. Kutokana na sababu hiyo, waliamua kuwa, ili kutekeleza nia yao hiyo, malezi ya vijana waliokuwa wakitaka kujiunga na Shirika, yafanyike kule kule Napoli, Italia.
Mapadre walilipokea wazo hilo kwa utayari, lakini wakati huo huo walikuwa wakikabiliwa na uhaba wa mapadre. Ijapokuwa wazo lilikuwa zuri, walishindwa kulitekeleza upesi kutokana na uhaba wa mapadre waliokuwa nao. Kutokana na sababu hiyo, waliamua kuwa, ili kutekeleza nia yao hiyo, malezi ya vijana waliokuwa wakitaka kujiunga na Shirika, yafanyike kule kule Napoli, Italia.
Sista Emmerensiana
Huwezi kuongelea Wakarmeli wa Utawa wa Kwanza nchini Tanzania bila kugusia Sr. Emmerensiana pamona na masista wengine Wakarmeli. Maana jukumu la kuwasiliana na kuwakusanya vijana liliwekwa mikononi mwa Masista wakiongozwa na Sista Emmerensiana. Vijana waliopiga hodi walielezwa lengo la mapadre na mpango mzima waliokuwa nao wa kutaka kufungua misheni hapa Tanzania. Wale waliokuwa tayari walikwenda Italia kwa ajili ya malezi na masomo ya falsafa na teolojia. Mapadre wakarmeli waitaliano walitaka Watanzania wawe wamisionari katika nchi yao wenyewe.
Mapadre wa kwanza Watanzania
Juhudi hizo zilianza kuzaa matunda mwaka 1999 pale Mkarmeli wa kwanza Mtanzania alipopewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 12.09, huko huko Napoli Italia. Huyu si mwingine bali ni Pd. Paulo Innocent Kaigalula, O.Carm. Mkarmeli wa pili Mtanzania kupewa Daraja Takatifu ya Upadre ni Pd. Thomas M. Mtey, O.Carm. ambaye alipadrishwa tarehe 19.11.2006 huko huko Napoli, Italia. Padre wa tatu ni Pd. Dominic M. Somola, O.Carm. aliyepadrishwa tarehe 24.08.2012 hapa hapa katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Vile vile kuna mapadre wengine watatu Pd. Paulo M. Malewa, O.Carm, Pd. Paschal M. Shirima, O.Carm. na Pd. Victor M. Biramata, O.Carm. Hawa watatu waliweka nadhiri za muda tarehe 13.09.2009 na wakaweka nadhiri za daima tarehe 05.12.2012 huko Napoli Italia. Walipewa Daraja Takatifu ya Ushemasi tarehe 4.1.2013 na Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo na kupewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 5.7.2013 na Mhashamu Askofu Titus Mdoe askofu msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Kufunguliwa nyumba
Baada ya kukamilisha malezi na maandalizi yaliyostahili, na kupokea baraka kutoka kwa Mkuu wa Komisarieti Pd. Alfredo M. Di Cerbo, tulianza safari ya kurejea tena Tanzania tukiwa tayari kwa ajili ya kufungua nyumba. Safari yetu ya kurejea Tanzania ilianza jioni ya tarehe 30.09.2009. Aliyekabidhiwa jukumu la kuongoza kundi letu la wamisionari wa “nyumbani” alikuwa ni Pd. Thomas M. Mtey, O.Carm.
Pd. Richard Munishi
Tuliondoka Italia tukiwa watu sita, mafrateri wanne na mpostulanti mmoja Richard Munishi. Baadae aliondoka na kujiunga Jimbo la Moshi na kupewa Daraja ya Upadre. Siku yetu ya kwanza kuwa hapa Tanzania kama wamisionari ilikuwa ni tarehe 01.10.2009, siku ambayo ni sherehe ya Mt. Teresia wa Mtoto Yesu msimamizi wa misioni zote duniani. Mt. Teresia wa Mtoto Yesu ni Mkarmeli.
Konventi yetu ilibarikiwa tarehe 08.10.2009 na aliyekuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaama, Mhashamu Methodius Kilaini. Tulianza kuishi rasmi katika konventi yetu tarehe 10.10.2009 baada ya kukaa kwa Masista Wakarmeli walioko Boko kwa wiki moja. Tarehe 30.11.2009 tulienda kujitambulisha kwa Kardinali Polycarp Pengo ambaye alitupokea kwa furaha na akatupa baraka zake za kibaba. Mpaka sasa kwenye jumuiya yetu tuko jumla ya mapadre watawa tano na walelewa wanne: Padre Thomas M. Mtey, O.Carm. Padre Dominic Somola M. Somola, O.Carm. Padre Paulo M. Malewa, O.Carm. Padre. Paschal M. Shirima, O.Carm na Padre. Victor M. Biramata, O.Carm.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.