Kanuni ya Albert

Mt. Albert wa Yerusalemu, Patriarka wa Yerusalemu kati ya mwaka 1206 na 1214 aliwapatia wamonaki wa kilatini waliokuwa wakiishi Mlima Karmeli kanuni ya maisha (formula vitae). Kanuni hii ilikubaliwa na Papa Onorio III tarehe 30.1.1226, halafu tena ikaidhinishwa na Papa Gregori IX tarehe 6.4.1229 na tena ikaidhinishwa na Papa Innocent IV tarehe 8.6.1245. Papa huyu wa mwisho hatimaye aliipitisha kanuni hiyo tarehe 1.10.1247 kwa sherehe kuwa kanuni ya kudumu ya shirika la kitawa la Wakarmeli. Kwa kupitishwa kanuni hiyo wamonaki walianza kutambulikana kuwa ni watawa rasmi. Baada ya hapo shirika limeendelea kukua na kusambaa sehemmu mbalimbali duniani.

“Propositum” ya Wakarmeli wa Kwanza

(Propositum maana yake mapendekezo).

1. Wakarmeli wanamwendea Mt. Albert

Wakarmeli walioishi mlima Karmeli walimwendea Mt. Albert –aliyekuwa Patriarka wa Yerusalemu wakimwomba awapatie Mwongozo wa maisha. Yeye aliwaambia wamempelekee mapendekezo ya jinsi wanavyotaka kuishi. Mapendekezo hayo ndiyo yanayoitwa “Propositum”.

2. Lengo- Mambo ya msingi katika Kanuni

Kanuni inasema kwamba ni suala la msingi kwa mkarmeli “kuishi maisha ya utii kwa Yesu Kristo -wenye moyo safi na katikadhamiri nzuri, kama ulazima wa kumwitikia Mwalimu” (namba 2.). Haisemi utii kwa papa au askofu au padre bali kwa Yesu Kristo. Hiki ni kitu cha kipekee kabisa na cha tofauti. Kuishi maisha ya utii kwa Yesu Kristo, kunawafanya wakarmeli wajifunge wao wenyewe hasa katika mambo yafuatayo:
kuendeleza  tafakari ya maisha yao, katika majadiliano ya wazi na Mungu
kuishi upendo kamili
kutafakari usiku na mchana Neno la Bwana
kusali pamoja au peke yake mara kadhaa kwa siku
kushiriki adhimisho la Ekaristi kila siku
kufanya kazi za mikono, kama Paulo Mtume alivyofanya 
kujisafisha/kujitakasa kwa kila namna dhidi ya uovu
Kuishi umaskini kwa kuweka pamoja vitu vinavyopatikana
Kulipendo Kanisa na watu wote
Kukubali matakwa yao yaendane na yale ya Mungu, kutafuta mapenzi ya Mungu daima katika imani, kwa kupitia mazungumzo na kupitia utambuzi (discernmen)wa maisha.

 

Kuwa na maisha yenye utaratibu

Toka mwanzo walikuwa na nadhiri ya kutorudi nyumbani kwao.
Huduma kwa Kristo – kuishi katika kumfuasa Yesu Kristo, “In Obsequio Iesu Christi”. Katika Propositum, anatajwa mtu aliyekuwa kama kiongozi wao, “B”.
Hivyo “Kanuni ya Maisha”, aliyowapatia Mt. Albert, ilitokana na Propositum yao.

3. Norma di Vita, Kanuni ya maisha

Maisha yao yalikuwa ya kimonaki lakini yakiwa na chembechembe za kijumuiya.
Yesu aliwekwa katikati ya maisha yao –kwa neno “obsequio”. Kumtegemea Yesu kwa kila kitu: Sura-7 na 18. Kristo kama nguvu Sura 10. Kutenda kadiri ya Nafsi ya Yesu 14. Matunda ya mfufuka Sura ya 9-10. Yote hayo yanafanyika katika ufunguo wa kitovu cha maisha ya  Utatu Mtakatifu Sura 8, 14,15.

Kanuni ya Karmeli kwa kiswahili

1.  Albert kwa neema ya Mungu, aliyetwa Patriarka wa Kanisa la Yerusalemu kwa wapendwa wana katika Kristo, B. na kwa waeremiti wengine walioko chini ya utii wake, wakaao kwenye chemchemi katika mlima Karmeli: salamu katika Bwana nabaraka za Roho Mtakatifu.
2. Mara nyingi na kwa njia nyingi mababa watakatifu waliweka jinsi kila mmoja katika shirika lolote au njia yoyote ya maisha ya kitawa aliyochagua anavyotakiwa kuishi katika utii kwa Yesu Kristo na kumtumikia kwa uaminifu kwa moyo safi na dhamiri njema.
3. Hata hivyo kwa kuwa mnahitaji kutoka kwetu kwa mujibu wa madhumuni yenu sisi tunawakabidhi ninyi kanuni ya maishaambayo mnatakiwa muifuate  katika siku zijazo.
4. Hiki katika nafasi ya kwanza tunakianzisha kwamba muwe na mkuu miongoni mwenu ambaye atachaguliwa katika ofisi hii kwa ridhaa moja ya yote au ya sehemu kubwa na yenye matashi mazuri, ambaye kila mmoja wenu amwahidi utii na apouahadiajifunze kuutekeleza kwa ukweli wa matendo pamoja na usafi wa moyo na kujikatalia kumiliki vitu.

5. Mnaweza tena kuanzisha makazi kwenye ueremiti au mahali mtakapopewa pakufaa na nafuu kwa ajili ya heshima ya shirika lenu kama ambavyo itakaonekana inafaa kwa mkuu na ndugu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.

Home

Kundi la Wakarmeli Watanzania wa kwanza lililofungua misheni 2009 Bikira Maria na Nabii Eliya katika Karmeli