Vocation

Wito ni nini?

Wito ni sauti (vox) anayoisikia mtu ndani ya nafsi yake ikimwita na kumwalika kuishi aina fulani ya maisha. Sauti hii hutoka kwa Mungu mwenyewe.

Wito wa kitawa ni nini?

 Wito wa kitawa ni neema ya pekee wanayopewa baadhi ya watu ndani ya Kanisa wanaoitwa kuishi maisha ya mashauri ya kiinjili.

Aina mbili za wito

1. Wito wa maisha -Kuitwa katika maisha ya ndoa, ya upadre, ya utawa au ya peke yako
2. Wito wa kazi -kwa mfano kuwa mwalimu, daktari, nesi, au polisi.
Watu huwa wanachanganya wanaposema kuwa wito wa upadre au utawa ni kama wito mwingine ule kama vile udaktari, au ualimu. Hilo si sahihi. Wito wa utawa au upadre ni wito wa maisha. Ndiyo maana hata watawa wana wito wa kazi nyinginezo kama vile udaktari, ualimu na kadhalika.

Wito mmoja wa utakatifu

Wote hawa wanaitikia wito mmoja wa utakatifu. Wote tuna wito mmoja wa kuwa watakatifu. Kila mtu huitikia wito huo kwa njia yake aliyopewa na Mungu. Ndipo hapo wengine wanakuwa wanandoa, wengine wanakuwa mapadre, wengine wanakuwa watawa, wengine wanabaki bila kuoa au kuolewa na si watawa wala mapadre (single).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.

Home

Kundi la Wakarmeli Watanzania wa kwanza lililofungua misheni 2009 Bikira Maria na Nabii Eliya katika Karmeli