Mwaka 1192 kundi la wamonaki wa kilatini (Wakarmeli) lilionekana katika mlima Karmeli karibu na "chemchem ya nabii Eliya", katika moja ya mabonde membamba ya Mlima Karmeli.
Bikira Maria wa Mlima Karmeli
Wakarmeli wana uhusiano wa kipekee na Bikira Maria na nabii Eliya. Shirika la Karmeli ni shirika la kimaria, nafasi yake katika maisha yao, inawafanya wamtambue kwa dhamiri zao kama, Dada, Mama na Mlezi wao. Wakarmeli wa kwanza walikuwa na dhamiri hiyo tangu walipoanza kuishi katika mlima Karmeli ndio maana walijenga Kanisa la kwanza kwa heshima yake. Nabii Eliya mkaa pweke
Wakarmeli wa kwanza waliishi maisha ya kieliya kiasi kwamba walijihisi kuwa naye moja kwa moja. Hawakuwa Wakarmeli tu waliokuwa wakivutwa na nabii Eliya bali hata mahujaji wengine wengi wa kipindi kile ambao walikuwa wakiitembelea Nchi Takatifu, walikuwa wakiguswa na maisha yake. Ni baba wa Wakarmeli. 
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.