MAELEKEZO MUHIMU NA MAHITAJI YA KUJIUNGA
NA SHIRIKA LA WAKARMELI TANZANIA
Elimu: Wanaotaka kujiunga na Shirika la Wakarmeli wanatakiwa wawe na cheti cha kidato sita kulingana na utaratibu na kanuni za Shirika na ufaulu wao ni lazima uwe wa Daraja la kwanza au la Pili au hata la Tatu lakini wawe na alama mbili, (Two principles) (au wawe na cheti cha chuo kikuu, au Taasisi za elimu ya juu). Hii ni kwa mujibu wa taratibu za kujiunga na Shirika la Wakarmeli na Chuo Kikuu cha Morogoro. Kipindi cha kuanza kujifunza maisha ya Karmeli huanza wiki ya mwisho wa Julai. Ni kipindi ambacho matokeo yao ya shule huchunguzwa na hujifunza maisha ya awali ya Wakarmeli. Barua ya maombi ya kujiunga na Shirika, kwa wale ambao baada ya miezi mitano ya majaribio wanajisikia ameitwa Karmeli, huandika barua ya kuomba kujiunga na Shirika kabla ya kwenda likizo fupi. Kwa muda huo Shirika hutathmini mwelekeo wao. Vijana hupewa taarifa ya kuitwa rasmi kujiunga na Shirika wakiwa nyumbani. Likizo yao huanza Desemba hadi Januari. Wanaporudi kutoka nyumbani, hutakiwa kuleta barua ya maoni kutoka kwa maparoko wao (Parokiani) (kama ni lazima), cheti cha kidato cha nne na kivuli cha matokeo ya kidato sita. Au matokeo mengine ya chuo kikuu au taasisi ya elimu ya juu. Toka mwezi wa kwanza hadi mwezi wa saba huendelea na mafunzo ya Shirika na ya Utawa kwa ujumla. Mwezi wa kumi huanza masomo ya falsafa.Malezi ya wanafunzi Wakarmeli wa kwanza nchini Tanzania
Mwaka huu wa 2016 tunatarajia kupokea vijana wengine.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.