Hali
ya maisha waliyoishi Wakarmeli wa kwanza ilikuwa ni ya kieliya kiasi kwamba
walijisikia kuwa katika hali ya kuwasiliana
naye moja kwa moja. Hawakuwa Wakarmeli tu waliokuwa wakivutwa na nabii
Eliya bali hata mahujaji wengine wengi wa kipindi kile ambao walikuwa
wakiitembelea Nchi Takatifu, walikuwa wakiguswa na maisha yake. Wengi wao
waliokuwa wakienda kuhiji Nchi Takatifu walikuwa wakifika pia mlima Karmeli
sehemu ambayo Eliya aliishi maisha ya kieremiti. Wakarmeli waliishi mlima
Karmeli karibu na chemchemi ya Eliya wakitamani kuwa kama yeye. Walimchagua
Eliya “mtu wa jangwa” kuwa kama baba yao na kiongozi wao wa kiroho.Eliya alikuwa ni mtu wa sala na aliishi katika uwepo wa
Mungu akimtumikia kwa uaminifu mkubwa. Hata pale wana wa Israeli
walipokengeuka, yeye alisimama imara akiitetea imani halisi ya Israeli, imani
kwa Mungu mmoja. Kwa maisha yake Eliya anamfundisha kila mmoja wetu jinsi ya
kuishi kwa vitendo upendo na imani kwa Mungu. Alipochagua kuishi maisha ya
kipweke, ni wazi alikuwa akimfundisha kila mtu njia sahihi ya kuzitawala tamaa za kimwili kwa ajili ya kuwa na moyo safi. Eliya aliishi maisha ya kifukara, maisha ya kijangwa, maisha ya kipweke
kwa utakatifu za wazi ulioonekana kwa watu wote (Soma YsB 48:1-11). Kutokana na
maisha yake ya kimonaki, anaheshimiwa sana na mababa wengi wa kimonaki ambao
wanamwona kuwa yeye ndiye “mwanzilishi”
wa maisha hayo. Kwa upande wetu Wakarmeli tunamheshimu kama baba yetu wa kiroho
na anatajwa katika vitabu vya kiliturujia vya Shirika.
Utume wake
Kazi
yake ukubwa ilikuwa kuwarudisha kwa Mungu wa ukweli waabudu miungu.
Biblia haitaji jina la baba yake wala la mama yake. Ni mfano wa
Melkisedeck.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.